Home » » Wanakijiji wa Babati wapatiwa mashine za Kukamua Ufuta

Wanakijiji wa Babati wapatiwa mashine za Kukamua Ufuta

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Baadhi ya wakulima wa vikundi vya Msange na Changamkeni wa Kijiji cha Vilima Vitatu, Kata ya Nkaiti, Tarafa ya Mbugwe, Wilaya ya Babati, Mkoani Manyara, wakijaribu mashine yao ya kukamulia ufuta baada ya kukabidhiwa jana na Ofisa Masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia, ambapo shirika hilo liligawa mashine 10 kwenye vikundi 18 vya wakulima wa Tarafa hiyo.
Wakulima wa vikundi vya Mkombozi na Shamabo wa Kijiji cha Shaurimoyo, Kata ya Nkaiti Tarafa ya Mbugwe, Wilaya ya Babati, Mkoani Manyara, wakijaribu mashine yao ya kukamua ufuta baada ya kukabidhiwa  na Ofisa Masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia, ambapo shirika hilo liligawa mashine 10 kwenye vikundi 18 vya wakulima wa Tarafa hiyo.
 Ofisa Masoko wa shirika la Farm Africa Rahel Pazzia, kulia akiwakabidhi mashine ya kukamua ufuta wana kikundi wa wakulima wa ufuta wa kikundi cha Faraja na Chemchem kwenye Kijiji cha Vilima Vitatu, Wilaya ni Babati Mkoani Manyara
 Wakulima wa ufuta wa vikundi vya Mkombozi na Shamabo wa Kijiji cha Shaurimoyo, Kata ya Mwada Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakiwa na mashine yao ya kukamulia ufuta iliyotolewa na shirika la Farm Africa, ambapo shirika hilo liligawa mashine 10 kwa vikundi 18 vya ufuta katika Tarafa ya Mbugwe.
Wanakikundi wa Sayuni na Mti wa maziwa, wakulima wa ufuta wa Kijiji cha Ngolley Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakiwa na mashine yao ya kukamua ufuta baada ya kukabidhiwa na Ofisa Masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia.
Picha na Michuzi Blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa