Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wamiliki wa migodi na wachimbaji wa madini ya Tanzanite, mji wa Mirerani mkoani Manyara, wametakiwa kuwekeza wilayani hapa.
Padri Pastory Kijuu wa Kanisa Katoliki, Parokia ya
Bikira Maria alitoa wito huo juzi alipozindua Shule ya Msingi na ya
Awali ya Blue Tanzanite.
Padri Kijuu alisema watu wengi wamekuwa wakipata
madini hayo na kwenda kuwekeza maeneo mengine, ikiwamo katika miji ya
Arusha na Moshi badala ya kunufaisha eneo husika.
“Sio sahihi hata kidogo kuja Mirerani kuchota
utajiri na kuondoka nao wote pasipo kuwekeza na kwenda kuwanufaisha
Ulaya, Afrika Kusini au kwingine na kusahau sehemu ulipopata mali,”
alisema Padri Kijuu.
Alisema mkurugenzi wa Shule ya Blue Tanzanite,
Alex Ombade anastahili pongezi kwa kujenga shule yenye walimu, majengo
mazuri na eneo kubwa.
Naye Ombade alisema shule yake ilianzishwa mwaka 2008 na hadi sasa ina wanafunzi 360.
“Lengo la kuanzishwa kwa shule hii ni kuhakikisha
jamii ya eneo hili inapata elimu bora itayowasaidia katika maisha yao,”
alisema Ombade.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji wa Mirerani, Albert
Siloli alisema Serikali ipo pamoja na taasisi binafsi zinazotoa huduma
kwa jamii na itaendelea kuziunga mkono ili kufanikisha maendeleo kwa
jamii.
“Tutaendelea kushirikiana na watu kama Ombade
ambao wamejitolea kuwekeza kwenye shule kwani watoto wetu wa Mirerani na
majirani zetu watapata elimu,” alisema Siloli.
Hata hivyo, mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo,
Magweiga Mack alisema Blue Tanzanite imezinduliwa kwa maombi na sala,
hivyo wanasubiri kuweka jiwe la msingi.
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment