Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wakulima wa Kijiji cha Galapo Wilayani Babati wakipakia mahindi yao kwenye magunia kwenye soko la Galapo Mkoani Manyara, jana.
Zaidi ya tani 7,400 za zao la mahindi zilizozalishwa na wakulima
wadogo wa kata za Galapo na Qash wilayani Babati mkoani Manyara
zimekosa soko na kurundikwa katika Soko la Galapo, eneo ambalo zinaweza
kuharibika wakati wowote.
Wakizungumza jana na mratibu wa Mtandao wa Vikundi
vya Wakulima wa Manyara (Mviwata), Martin Pius alisema wakulima hao
waliiomba Serikali kufanya jitihada za haraka kwa kununua mahindi hayo
ili kunusuru hasara kwa wakulima wa eneo hilo.
Mkulima wa Kijiji cha Galapo, Dodo Ekwani alisema
wakulima wanateseka kwa kukosa fedha za kuwalipia ada watoto wao, kupata
huduma za afya na pia kulipa vibarua na wakikosa viongozi wa kuwatetea
juu ya hilo.
Mwenyekiti wa soko hilo, Lohay Langai alisema
wakulima wa vijiji vya Galapo, Gedamary, Qash na Halu walileta mahindi
yao sokoni wakitegemea Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula nchini
(NFRA) wangenunua, lakini hali imekuwa tofauti.
Diwani wa Kata ya Galapo, Michael Naas Dil alisema
suala hilo limekuwa kero katika kata yake na inampa wakati mgumu akiwa
sehemu ya uongozi, hivyo ameiomba Serikali itoe fedha haraka kwa NFRA
ili waweze kununua mazao hayo.
Mratibu wa Mviwata wa mkoa huo, Pius alisema soko
ni suala muhimu na kichocheo kikubwa kwa uzalishaji na ubora wa mazao ya
kilimo na inaweza kuwafanya wakulima wazalishe mazao mengi na kwa ubora
unaohitajika.
“Hivi karibuni Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,
Chakula na Ushirika ilisaini mkataba na Kenya ili kununua mahindi ya
wakulima, hivyo mchakato huo ufanywe haraka na taarifa ziwekwe wazi ili
wakulima wadogo wafaidike,” alisema Pius.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment