CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Taifa kimetoa siku 10 kwa uongozi wa chama hicho
Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara kufanya uchaguzi ngazi ya chini hadi
wilaya ili waweze kupata tiketi ya kushiriki uchaguzi mkuu wa 2015.
Mkuu wa Itikadi na
Uenezi Taifa, Waitara Mwita akizungumza na kamati ya utendaji ya chama
hicho wilayani Kiteto hivi karibuni alisema, ushiriki wa chama hicho
uchaguzi mkuu 2015 utategemea kukamilika kwa uchaguzi ngazi ya chini.
"Hatutaivumilia wilaya
yoyote ishiriki uchaguzi mkuu mwakani, kama hawatafanya uchaguzi ndani
ya chama na hili tutalisimamia kikamilifu na wala hatutaona haya
kulisemea na mahali popote nchini,"alisema
Wakati huo huo, kwa
mujibu wa Katiba ya CHADEMA kiongozi huyo ameufuta uongozi wa vijana
wilaya baada ya kuonekana wana umri mkubwa na kuchaguliwa Abubakari
Kidevu kuwa Mwenyekiti huku Katibu akiwa Athumani Ismail.
Mbali na hatua hiyo pia
kura zililazimika kupigwa kuhusu kuvunja kamati ya utendaji ama
kutovunjwa kutokana na kuonekana kushindwa kuwajibika ipasavyo ambapo
walilazimika kuongezewa wajumbe wengine ili kusukuma mbele shughuli za
chama.
"Hali haikuwa shwari
kwenye kikao, kwani hata kamati ya utendaji ilitakiwa kuvunjwa kutokana
na sababu mbalimbali zikiwemo za kutowajibika ipasavyo hali
iliyosababisha kudorora kwa chama kipindi chote,"alisema Ole Loilole
Leng'isya Katibu wa Wilaya.
Aidha, Katibu huyo
alisema chama kilitakiwa kufanya uchaguzi huo Juni 30, mwaka huu na
kwamba kutokana na sababu mbalimbali zilichangia kutofanyika.
Alitaja baadhi ya
sababu hizo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa amani katika maeneo mengi
ya Wilaya ya Kiteto juu ya migogoro ya ardhi ambayo inaendelea hadi sasa
na kusababisha madhara yakiwemo mauaji.
Alisema, hali hiyo
imekuwa tishio kwa wananchi na hata viongozi wa kisiasa na Serikali kwa
ujumla kuendelea kufanya kazi katika mazingira hayo kutokana na kitendo
cha mauaji ya kila mara huku kukiwa hakuna jitihada za makusudi
kukabiliana na tatizo hilo.
Hata hivyo, CHADEMA kwa
pamoja wamelaani mauaji yanayoendelea kujitokeza kwa jamii ya wakulima
na wafugaji wilayani humo na kuitaka Serikali kuzuia ili kuwapa wananchi
waweze kufanya kazi ya ujenzi wa
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment