Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akijibu swali
toka kwa Mheshimiwa Martha Umbulla ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum
lililokuwa likiuliza ni lini Serikali itasikiliza kilio cha muda mrefu
na kujenga Senta ya michezo ya riadha mkoani Manyara ili vijana wengi
wenye vipaji waweze kunufaika, leo Bungeni mjini Dodoma.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.
Serikali
inaendelea kuendeleza sekta ya michezo nchini ikiwemo kutafuta maeneo
ya kuwawezesha vijana kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana
ikiwemo kuwapatia ajira vijana.
Kauli
hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati akijibu swali toka kwa
Mheshimiwa Martha Umbulla ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum lililokuwa
likiuliza ni lini Serikali itasikiliza kilio cha muda mrefu na kujenga
Senta ya michezo ya riadha mkoani Manyara ili vijana wengi wenye vipaji
waweze kunufaika.
Mhe.
Nnauye amesema kuwa Mkoa wa Manyara pamoja na Wilaya zake una vijana
wenye vipaji vya riadha na michezo ambapo Serikali inatambua pia umuhimu
wa kuwa na kituo kikubwa cha michezo hasa ya riadha ambacho pamoja na
mambo mengine kitasaidia kuibua, kukuza na kuviendeleza vipaji vya
vijana ikiwa ni pamoja na kuwapatia ajira vijana mkoani humo.
Amesema
kuwa, Serikali ya Mkoa wa Manyara imepanga kujenga Kituo cha Michezo
cha Mkoa, mara bada ya kukamilisha mazungumzo na kukiubaliana na
wananchi wanaomiliki ardhi mkoani humo.
Aidha,
ameeleza kuwa kwa kipindi hiki ambacho Uongozi wa mkoa hauna Kituo cha
Michezo, mkoa umepanga kutumia kambi ya michezo ya Hifadhi ya Taifa ya
Tarangire kwa muda, wakati wanasubiri kupatikana kwa eneo la kudumu la
mkoa.
“Hii
inatokana na sababu kuwa hifadhi ya Taifa ya Tarangire ina hosteli za
kutosha na viwanja vya michezo vya kutosha”, alisema Mhe. Nnauye.
Aliongeza
kuwa, kujengwa kwa kituo hicho kutaongeza ajira na kupanua shughuli za
kibiashara na hata kukua kwa uchumi wa mkoa wa Manyara.
“Serikali inaendelea na mazungumzo na wananchi wamiliki wa ardhi ili kupata eneo la ujenzi”, aliongeza Mhe. Nnauye.
Kwa
upande mwingine ameziomba Halmashauri kuisadia Serikali katika kulinda
maeneo ya michezo ambayo baadhi ya watu pasipo utaaratibu wanavamia na
kugeuza kuwa maeneo yao ya kufanyia shughuli zao ikiwemo makazi.
0 comments:
Post a Comment