Home » » WAZEE BABATI WAIANGUKIA SERIKALI

WAZEE BABATI WAIANGUKIA SERIKALI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

dsc03289
Na JANETH MUSHI- BABATI
SERIKALI imeombwa kujenga zahanati katika kituo cha kulelea wazee wasiojiweza katika Kata ya Magugu, wilayani Babati, Mkoa wa Manyara.
Ombi hilo lilitolewa hivi karibuni na wazee hao ambao walisema kutokana na eneo hilo kutokuwa na zahanati wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Mmoja wa wazee hao, Joseph Apolinary, alisema licha ya ukosefu wa zahanati katika kituo hicho, pia kituo chao hakina gari la kubeba wagonjwa, jambo linalowalazimu kutumia gharama kubwa kukodisha usafiri ikiwamo kupanda pikipiki pindi wanapohitaji huduma za afya.
“Tunaiomba Serikali ijenge zahanati kituoni hapa au karibu na eneo hili ili tunapohitaji huduma ya afya tuipate kwa wakati.
“Pia tunaomba gari la wagonjwa kwani kutokuwapo kwa gari hilo, kunatulazimu wakati mwingine kupanda pikipiki ingawa umri wetu hauruhusu kabisa kupanda pikipiki,” alisema Aporinary.
Naye mkuu wa kituo hicho kiitwacho Makao, Samson Munuo, alisema wamekuwa wakitembelewa kituoni hapo mara moja kwa wiki na madaktari ila wakati mwingine inapotokea dharura wakati wa usiku, wanapata shida kutokana na kukosekana kwa usafiri.
“Tunatembelewa na madaktari mara moja kwa wiki ila umbali wa kituo cha afya umekuwa changamoto hasa nyakati za usiku kunapotokea mgonjwa.
 CHANZO GAZETI LA MTANZANIA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa