Mtaalam wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Mhandisi Emillian Nyanda (kushoto) akibadilishana mawazo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uzalishaji wa Umeme kwa
kutumia Maji ya Darakuta, Raphael Bapsl mara baada ya wataalam wa
nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini kuwasili wilayani
humo kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme.
Na Greyson Mwase, Manyara.
Imeelezwa kuwa kampuni ya uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji
(Darakuta Hydro Power Project) iliyopo Babati mkoani Manyara
inatarajia kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka Kilowati 370 hadi
Megawati 1.3 zitakazoingizwa kwenye Gridi ya Taifa na kupunguza
upungufu wa umeme nchini ifikapo mwaka 2021.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Raphael
Bapsl wilayani Babati mkoani Manyara wakati wa ziara ya wataalam
wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika wilaya hiyo,
yenye lengo la kuangalia maendeleo ya miradi ya uzalishaji umeme na
kubaini changamoto zake.
Akielezea historia ya mradi huo, Bapsl alisema kampuni yake ilianza
kuzalisha umeme wa Kilowati 50 mwaka 1995 na kuongeza kuwa Aprili
mwaka 2016 kampuni ilianza kuliuzia Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) umeme unaoingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
Alisema mbali na umeme huo kutumika kwa matumizi ya nyumbani
ambao ni kidogo hususan katika shughuli za kilimo na ufugaji ili
kujiongezea kipato, kampuni yake huuza umeme wa ziada kwa
TANESCO ili kuongeza kiasi cha umeme katika wilaya ya Babati.
Alisisitiza kuwa ili Tanzania kuingia katika uchumi wa kati kupitia
uwekezaji kwenye viwanda, nishati ya umeme wa uhakika inahitajika na
kuendelea kusema kuwa kwa kutambua hilo kampuni yake imeweka
mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ili kuhakikisha inachangia katika
ongezeko la umeme katika Gridi ya Taifa.
Mtaalam wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Mhandisi Emillian Nyanda (kushoto) akibadilishana mawazo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uzalishaji wa Umeme kwa
kutumia Maji ya Darakuta, Raphael Bapsl mara baada ya wataalam wa
nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini kuwasili wilayani
humo kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme.
Sehemu ya kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia maji cha Darakuta
kilichopo wilayani Babati mkoani Manyara.
Mtaalam wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Mhandisi Emillian Nyanda ( wa pili kutoka kulia) na Thomas Ndazi ( wa
kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa
kampuni ya Darakuta mara baada ya kumalizika kwa ziara katika
kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uzalishaji wa Umeme kwa
kutumia Maji ya Darakuta, Raphael Bapsl (katikati) akionesha moja ya
chanzo cha maji kinachotumika katika kuzalisha umeme.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uzalishaji wa Umeme kwa
kutumia Maji ya Darakuta, Raphael Bapsl (kushoto) akielezea mitambo
ya kuzalisha umeme inavyofanya kazi katika kituo hicho kwa Mtaalam
wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
Emillian Nyanda (kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uzalishaji wa Umeme kwa
kutumia Maji ya Darakuta, Raphael Bapsl (katikati) akionesha mfumo
wa kuongozea mitambo ya kuzalisha umeme ya kituo hicho.
0 comments:
Post a Comment