Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizugumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa
Manyara, Dkt. Joel Bendera wakiwa
katika kijiji cha Lembapuli kilichopo kwenye mpaka wa wilaya ya Kiteto
na Kilindi Januari 18, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alikwenda Kiteto na
Kilindi kutatua mgogoro wa mpaka unaovikabili vijiji vya Mafisa na
Kijungu. Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Muu wa Wilaya
ya Tanga mjini , Thobias Mwilapwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea kwenye moja ya jiwe la mpaka wa
wilaya ya Kilindi na Kiteto wakati alipokwenda kwenye kijiji cha
Lembapuli kilichopo kwenye mpaka wa Kiteto na Kilindi kutatua mgogoro
wa mpaka Januari 18, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara,
Dkt. Joel Bendera na kulia kwake ni Mkuu wa wilaya na Tanga na Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa watalaam wa upimaji
ardhi kuhusu jiwe la alama ya mpaka wa wilaya ya Kilindi na Kiteto
katika kijiji cha mpakani cha Lembapuli Januari 18, 2017. . Kushoto
kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na kulia kwake ni
Mkuu wa wilaya na Tanga na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias
Mwilapwa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu ramani inayoonyesha
mpaka wa wilaya ya Kilindi na Kiteto katika kijiji cha mpakani cha
Lembapuli wakati alipokwenda kutatua mgogoro wa mpaka kati ya wialya
hizo Januari 18, 2017. Mheshimiwa Majaliwa apia alifuatana na Mawaziri
, William Lukuvi wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi na George
Simbachawene wa Ofisi ya Rais- TAMISEMI.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Kiteto na Kilindi wakati
alipokwenda kwenye kijiji cha Lembapuli kilichopo kwenye mpaka wa
wilaya hizo kutatua mgogoro wa mpaka Januari 18, 2017. Wapili kushoto
ni Mkuu wa mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na wapili kulia ni Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutanao wa hadhaa katika kijiji cha
Lembapuli kilichopo mpakani mwa wilaya za Kilindi na Kiteto
alikokwenda kutatua mgogoro wa mpaka Januari 18, 2017.
Baadhi ya wananchi wa wilaya za Kilindi na Kiteto wakimshangilia
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara
katika kijiji cha Lembapuli kilichopo mpakani mwa wilaya za Kiteto na
Kilindi alikokwenda kutatua mgogoro wa mpaka Januari 18, 2017. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU AMALIZA MGOGORO WA MPAKA KILINDI NA KITETO
*Awaonya viongozi wa siasa wasiwavuruge wananchi
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameumaliza mgogoro wa mpaka wa ardhi baina ya
vijiji vya wilaya za Kiteto na Kilindi uliodumu kwa muda mrefu.
Mgogoro
huo ambao ulianza kusuluhishwa tangu mwaka 1997, umepata suluhu kwenye
mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu na kuwajumuisha Wakuu wa
Mikoa hiyo miwili, Wabunge wa Kiteto na Kilindi, wenyeviti wa
Halmashauri na madiwani wa kata mbili za mpakani pamoja na wananchi wa
kata hizo.
Waziri
Mkuu pia amewataka wanasiasa na viongozi wengine kutowavuruga wananchi
na badala yake wawaongoze vizuri na kutoa maelekezo kwa mujibu wa sheria
za nchi.Ametoa
agizo hilo leo (Jumatano, Januari 18, 2017) wakati akizungumza na
wananchi wa wilaya za Kiteto na Kilindi katika kijiji cha Lembapili
wilayani Kiteto, mkoani Manyara ambako ni kuna mpaka wa wilaya hizo
mbili alipokwenda kutatua mgogoro huo.
Amesema
viongozi wa wilaya hizo lazima wafuate sheria na wawaelekeze wananchi
umuhimu wa kuzingatia sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kuheshimu mipaka
iliyowekwa kwa mujibu wa sheria ili kuepusha migogoro.
Akizungumzia
kuhusu mgogoro huo wa mpaka, Waziri Mkuu amesema nchi ilishaweka mipaka
ya mikoa na wilaya zake yote tangu zamani na kumbukumbu zipo zikiwemo
za mpaka wa wilaya hizo tangu mwaka 1961 kwa tangazo la Serikali namba
65 na hakuna mabadiliko. Hivyo, aliwasisitiza wauheshimu na kuufuata.
Amesema
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
itakwenda kuweka alama vizuri na viongozi wa wilaya hizo
watashirikishwa. Alama hizo zitawekwa na kifaa maalumu, hivyo amewataka
wahusika watoe ushirikiano.
Waziri
Mkuu amesema katika kipindi ambacho Serikali itakuwa ikiweka alama
hizo, wananchi waendelee na shughuli zao hadi hapo zoezi
litakapokamilika na wala wasibughudhiwe.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa siku nane kwa watu wote wanaomiliki
silaha katika wilaya za Kilindi na Kiteto wazipeleke kwenye vituo vya
Polisi ili zisajiliwe upya na kisha Wakuu wa Mikoa wafanye operesheni
maalum na atakayekutwa anamiliki silaha kinyume cha sheria achukuliwe
hatua.
“Wakuu
wa Mikoa fanyeni ukaguzi maalum na atakayekutwa anamiliki silaha
kinyume na utaratibu achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria. Pia kuna
watu wana mitambo ya kutengenezea bunduki hapa, nao pia waisalimishe
haraka,” amesisitiza.
Kwa
upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw.
William Lukuvi amesema mwanzoni mwa Februari wataalamu wake watakwenda
katika mpaka huo ili kuanza kuweka alama vizuri.
Amesema
baadhi ya viongozi huwa wana tabia ya kuzuia watendaji kutekeleza
majukumu yao, hivyo ametumia gursa hiyo kuwaomba viongozi wa wilaya hizo
watoe ushirikiano.
Amesema
moja ya majukumu aliyopewa na Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli
ni kuhakikisha ndani ya miaka hii mitano anamaliza migogoro ya ardhi
nchini ukiwemo huo wa Kilindi na Kiteto.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, JANUARI 18, 2017.
0 comments:
Post a Comment