Home » » Diwani wa CCM Mbulu ajiuzulu

Diwani wa CCM Mbulu ajiuzulu

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Diwani maarufu wa CCM wa Kata ya Endamilay, wilayani Mbulu Mkoa wa Manyara, Gesso Bajuta ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo.
Bajuta ambaye amekuwa akitajwa kuwania ubunge wa Jimbo la Mbulu kupitia CCM mwaka 2015, jimbo ambalo sasa mbunge wake ni Mustapha Akoonay wa Chadema aliyetangaza uamuzi huo jana.
Akizungumza na gazeti hili jana, Bajuta ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa dawa za mifugo na kilimo alisema, amejiuzulu kutokana na kuchoshwa kuingiliwa katika utendaji kazi wake katika kata hiyo.
Bajuta alisema, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Lucas Ole Mukusi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa wilaya hiyo, Flatry Maasay wamekuwa wakimwingilia katika utendaji kazi wake.
Alisema viongozi hao, wamekuwa wakifanya vikao vya uchochezi katika kata yake na hivyo kufanya ashindwe kutimiza majukumu yake ya kuwasaidia wananchi katika kuleta maendeleo na kusisitiza kuendelea kushirikiana nao.
Katika kata hiyo, diwani huyo tayari amewezesha kufanikisha kwa ujenzi wa shule ya msingi na sekondari pia ameanzisha miradi ya ufugaji ng’ombe wa kisasa. Diwani maarufu wa CCM wa Kata ya Endamilay, wilayani Mbulu Mkoa wa Manyara, Gesso Bajuta ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo.
Bajuta ambaye amekuwa akitajwa kuwania ubunge wa Jimbo la Mbulu kupitia CCM mwaka 2015, jimbo ambalo sasa mbunge wake ni Mustapha Akoonay wa Chadema aliyetangaza uamuzi huo jana.
Akizungumza na gazeti hili jana, Bajuta ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa dawa za mifugo na kilimo alisema, amejiuzulu kutokana na kuchoshwa kuingiliwa katika utendaji kazi wake katika kata hiyo.
Bajuta alisema, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Lucas Ole Mukusi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa wilaya hiyo, Flatry Maasay wamekuwa wakimwingilia katika utendaji kazi wake.
Alisema viongozi hao, wamekuwa wakifanya vikao vya uchochezi katika kata yake na hivyo kufanya ashindwe kutimiza majukumu yake ya kuwasaidia wananchi katika kuleta maendeleo na kusisitiza kuendelea kushirikiana nao.
Katika kata hiyo, diwani huyo tayari amewezesha kufanikisha kwa ujenzi wa shule ya msingi na sekondari pia ameanzisha miradi ya ufugaji ng’ombe wa kisasa.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa