Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KATIKA
jitihada za kutatua changamoto za mitaji nchini kwa wajasiriamali
wadogo na wa kati, soko la hisa la Dar es Salaam limeanzisha soko la
kukuza ujasiriamali ambalo litawahudumia wajasiriamali wadogo na wale wa
kati katika kurahisisha upatikanaji wa mitaji wanayohitaji.
Ameyasema
hayo Bw. Emmanuel Nyalali kutoka Soko la Hisa la Dar es Salaam (EGM)
wakati akizungumza na wadau wa biashara wilayani Babati mkoani Manyara
katika semina ya soko la kukuza ujasiriamali, ambapo amedai kwamba soko
la kukuza ujasiriamali yaani (EGM) linatoa suluhu kwa changamoto
zinazowakabili wajasiriamali katika upatikanaji wa uhakika wa mitaji ya
muda mrefu kwa ajili ya kuendeleza biashara zao.
Aidha, Nyalali
alisema kwamba makampuni madogo na ya kati (SMEs) mengi yanayofanya
biashara hayana mazoea ya kuweka vizuri rekodi za biashara zao na hiyo
huleta changamoto katika kufanya makadirio ya mitaji na mauzo.
Pia
alisema kwamba changamoto kuu zinazokwaza maendeleo ya makampuni madogo
na kati (SMEs) ni kutokuwepo kwa mazingira mazuri ya kibiashara, ukosefu
wa ujuzi katika uendeshaji na usimamizi wa biashara pamoja na ukosefu
wa upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya ukuzaji wa biashara.
Awali,
akifungua semina ya wadau hao,Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bw. Elastol
Mbwilo alilitaka soko la hisa kuhakikisha linatoa elimu ya kutosha hadi
ngazi ya chini badala ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara wakubwa pekee
ili wapate kutambua umuhimu wa soko la hisa ambalo litasaidia
kubadilisha uchumi wao kwa haraka.
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment