Home » » FAHAMU KWA UNDANI HISTORIA YA MKOA WA MANYARA

FAHAMU KWA UNDANI HISTORIA YA MKOA WA MANYARA

image
image
Mkoa wa manyara ni moja ya mkoa uliopo kaskazini mwa  Tanzania pia Mkoa wa Manyara ni kati ya mikoa 26 za Tanzania . Babati ndiyo makao makuu ya mkoa .
              MIPAKA
Umepakana na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa mashariki, Mkoa wa Dodoma upande wa kusini na mikoa ya Singida na Shinyanga upande wa magharibi.
                    CHIMBUKO LAKE
Mkoa wa Manyara umetengwa na Mkoa wa Arusha mwaka 2002 kwa azimio la rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
           UKUBWA WAKE
Mkoa wa Manyara una eneo la km² 46,359.
            IDADI YA   Wakazi wa mkoa
Jumla ya wakazi mkoani ilikuwa 1,425,131 katika sensa ya mwaka 2012. Idadi hiyo imepatikana katika wilaya zifuatazo (idadi ya wakazi katika mabano mwaka 2002): Babati (303,013), Hanang (205,133), Mbulu (237,882), Simanjiro (141,676) na Kiteto (152,757). Sensa zinaonyesha kuonyesha kwamba ni kati ya mikoa ya Tanzania yenye ongezeko kubwa la wakazi.
             Sifa za mkoa Huu
Mkoa huu ni kati ya mikoa yenye maambukizi machache zaidi ya Ukimwi .
               MAKABILA YA MKOA NI
Wenyeji wa mkoa huu ni pamoja na Wairaqw, Wamasai , Wasonjo , Wafyomi na Wabarbaig wakijihusisha
        SHUGHULI ZA MKOA NI
shughuli za kilimo
image
na ufugaji kama njia ya kuingiza kipato chao cha kila siku. Mkoa huu unayo majimbo ya uchaguzi yanayofikia (6) ambayo yanajumuisha majimbo ya BabatI (V) BABATI  (M) Kiteto, Hanang, Mbulu na Simanjiro. Wilaya Kuna wilaya zifuatazo: Mbulu, Babati, Hanang, Simanjiro and Kiteto. Kwa maelezo zaidi ya mkoa tembeleaaHapa

CHANZO MANYARA KWANZA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa