Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kumekuwepo
na upotoshaji wa mafunzo ya utarajali (Internship programme) bila malipo yaani
fedha za kujikimu wakati wa mafunzo hayo kwa baadhi ya wanaotarajia kuanza
mafunzo kwa vitendo mapema mwaka huu.
Wizara
ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inapenda kuwajulisha kwamba
kwa sasa hakuna ‘intern’ aliyepangiwa kuanza mafunzo hayo kwani tunasubiri
watoke waliopo kwenye mafunzo.
Barua
iliyodukuliwa na kusambaa kwa lengo la kupotosha wataraji hao ilikuwa ni kwa
ajili ya wataraji (intern) kutoka nje ya nchi ambao kwa sheria hawalipiwi na
Serikali ya Tanzania.
Aidha
wapo ‘intern’ wawili ambao wanasoma nchini China na mwingine Algeria masomo yao
yalihitaji mafunzo kwa vitendo kabla ya kumaliza na kwa kuwa ilikua lazima
warudi vyuoni mwezi Oktoba waliomba kufanya mafunzo hayo kwa kujigharimia pamoja na kuwa ni watanzania na wazazi wao
walikuwa wameridhia hilo kwa maandishi ili warudi mapema kumalizia program yao ya udaktari.
Hivyo
ni watanzania wawili tu wameshapata barua yenye kuwataka kujilipia kwa mazingira hayo hakuna wengine
waliyepewa barua ya kuruhusiwa kwenda mafunzo ya utarajali (internship) bila
malipo.
Imetolewa
na;
Nsachris
Mwamwaja
Mkuu Kitengo cha Mawasiliano
Serikali-Afya
30/7/2017
0 comments:
Post a Comment