MAAFISA HABARI,MAWASILIANO NA UHUSIANO SERIKALINI WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Lango Kuu la Kuingia Hifadhi ya Taifa ya Tarangire iliyopo mkoani Manyara .
Mkuu wa Idara ya Utalii,Mhifadhi Theodora Aloyce akitoa maelezo kwa Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusino Serikalini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire iliyopo mkoani Manyara kwa lengo la kutangaza Utalii wa ndani.
Baadhi ya Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakiwa katika gari wakati wa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire kujionea vivutio mbalimbali vilivyoko katika Hifadhi hiyo wakiwemo Wanyama mbalimbali.
Miti Mikubwa ya Mibuyu ni sehemu ya Vivutio vilivyoko katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Digi Digi ni mmoja kati ya Wanyama wanaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ambaye Maafisa Habari wa Taasisi za Serikali walipata fursa kumuona.
Mnyama Simba akiwa katika muinuko ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ili kumrahisishia kuweza kuona maeneo ya mbali.
Twiga ni miongoni mwa wanyama ambao pia walionekana kwa uzuri zaidi katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Baadhi ya Maafisa Habari wa Taasisi za Serikali wakifurahia ziara ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ikiwa ni pamoja Stori walizokuwa wakipatiwa na waongoza watalii .
Kundi la Swala wakipata malisho ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Tumbili ni miongoni mwa wanyama walioko katika Hifadhi ya Tarangire.
Maafisa Habari wa Taasisi mbalimbali za Serikali wakichukua Taswira katika eneo la Picnic ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Makundi Makubwa ya Tembo ni kivutio kikubwa zaidi katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Baada ya Ziara ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire iliyopo mkoani Manyara ,Maafisa Habari wa Taasisi za Serikali wakachukua Taswira  na Mkuu wa Idara ya Utalii katia Hifadhi ya Taifa ya Tarangire Theodora Aloyce.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

TAGCO WAIKUMBUKA SHULE YA FAMILIA YA MZEE LAIBON ILIYOPO MTO WA MBU MKOANI MANYARA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusuano Serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Laiboni iliyopo Mto wa Mbu mkoani Manyara ,Rashid Mohamed msaada wa Madaftari 2500 kwa ajili ya wananfunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Mwenyekiti wa TAGCO ,Pascal Shelutete na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ,Dkt Hassan Abbas wakigawa Daftari kwa wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Loibon.
Mwenyekiti TAGCO ,Pascal Shelutete akizungumza mara baada ya kukabidhi Msaada huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusuano Serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete akipeana mkono na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Laibon ,Rashid Mohamed wakati akikabidhi msaaada wa Matenki mawili ya kuhifadhia maji shuleni hapo .kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo.
Mwenekiti wa TAGCO ,Pascal Shelutete akizungumza jambo na Wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Loibon.
Moja ya majengo ya Shule ya Msingi Loibon iliyojengwa na Mfugaji wa Jamii ya Kimaasai,Loibon Ole Mapii baada ya Mungu kumjalia watoto Zaidi ya 200 na wajukuu Zaidi ya 400 na kulazimika kujenga shule kwa ajili ya familia yake.
Wenyeji wa eneo ilipo shule hiyo Jamii ya Wafugaji wa Kimasaai waliandaa Nyama kwa ajili ya ugeni uliotembelea shule hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari,Mawasilianona Uhusiano Serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete na maafiwa Habar wenzake wakingojea kipande cha nyama .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Arusha.

Wananchi wamgomea mkuu wa wilaya

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wananchi wa Kijiji cha Langai, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wamemgomea Mkuu wa wilaya hiyo, Zephania Chaula kugawa ardhi yao wanayodai kuimiliki kihalali.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara jana Machi 18, 2018, wananchi hao wanaojishughulisha na kilimo na ufigaji wamesema hatua hiyo ya mkuu wa wilaya ni ubaguzi.
Mmoja wa wananchi hao, Paulo Simtek amesema wafugaji wamekuwa wakiishi eneo hilo kwa muda mrefu, lakini kitendo cha mkuu wa wilaya kuchukua mashamba yao, kuyamega na kuwapatia wakulima kunaweza kuibua migogoro.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Langai, Mathayo Ole Silongoi amesema kuwa sintofahamu hiyo inatokana na wa uongozi wa wilaya kudharau Serikali ya kijiji na kufanya uamuzi usiowahusu kwani mashamba hayo yako chini ya Serikali ya kijiji.
Akizungumzia suala hilo, Chaula amesema uongozi wa kijiji hicho umekuwa na ubaguzi wa jamii na ndicho chanzo cha migogoro na kwamba, Serikali itachukua hatua za kisheria dhidi yao ikiwemo kutoitisha mikutano ya kijiji tangu walipochaguliwa.
"Huo uongozi wa kijiji hatua za kisheria zinawafuata kwa kukiuka ya uongozi wao waache kusema nimegawa ardhi, bali waseme wao wamefanya nini ikiwemo kuitisha mikutano kusikiliza kero za wananchi na kusoma mapato na matumizi zaidi wanayoyafanya ni kuendekeza ubaguzi wa ukabila," amesema Chaula
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Jakson Siptek amesema wameanza kuchukua hatua za utatuzi na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati hatua zinaendelea.

Chanzo: Mwananchi

HALI YA UHARIBIFU WA MISITU HANANG,MKOANI MANYARA INAKUWA KWA KASI KUBWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Teddy Athumani(wa kwanza kutoka kulia)akipitia makabrasha ya mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang kujiridhisha namna watendaji wa Halmashauri wanavyotekeleza ilani ya chama tawala.
 Mbunge wa jimbo la Hanang,Mkoani Manyara,Dk.Mary Nagu (wa pili kutoka kulia) akipitia taarifa ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu iliyowasilishwa kwenye mkutano huo na kisha kutaka kufahami shilingi milioni 300 zilizoagizwa kwenye mkutano wa LAC Dodoma zitalipwa lini ili vikundi vya wanawake,vijana na walemavu viweze kunufaika na kujiongezea mitaji yao.
 Mkuu wa wilaya ya Hanang,Sara Msafiri akisisitiza jambo kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
 Katibu wa vikao vya Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Stevine Yonah(wa kwanza kutoka kushoto) akinukuu maazimio yote ya mkutano wa Baraza hilo ili watendaji waweze kutekeleza kikamilifu maazimio hayo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
 
 
Na,Jumbe Ismailly HANANG       Machi,01,2018        Mazingir
KUTOKANA na hali ya uharibifu wa misitu katika wilaya ya Hanang kuwa kubwa sana,Mkuu wa wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Sara Msafiri ameziagiza kamati za maendeleo za kata kujenga utamaduni wa kujadili katika vikao vyao juu ya hali ya uhifadhi wa misitu katika maeneo yao.
Akitoa agizo hilo kwenye mkutano wa kawaida wa Baraza la kawaida la madiwani wa Halmashauri hiyo,Mkuu wa wilaya huyo aliyataja baadhi ya maeneo ya vijiji vya Lalaji.Balangida na maeneo mengine hali ya mazingira ni mbaya sana.
“Kwa hiyo niwaombe kwamba kamati za maendeleo za kata mjadili na hali ya hifadhi ya misitu na ninazo taarifa za kutosha na nimejirisha wapo viongozi wengine  ni wa kisiasa wanashiriki katika biashara ya kukata miti,kuchoma na kuuza mkaa.”alisisitiza Mkuu huyo wa wilaya.
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya kupitia serikali kuu wameshatoa maagizo kwa watendaji kwamba mtu yeyote tule atakayetaka kukata miti hata kama aliupanda mwenyewe ni lazima apate kibali kutoka kwa Mkuu wa wilaya.
Hata hivyo Sara alisisitiza kwamba ni ukweli usiopingika na alioufanyia uchunguzi wa kina na kujiridhisha kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa,wakiwemo madiwani,wenyeviti wa vijiji,vitongoji na watendaji wanajihusisha na biashara ya kukata micti kuchoma mkaa na kuuza mazao hayo.
Akimpongeza Mkuu huyo wa wilaya,Mbunge wa jimbo la Hanang,Dk.Mary Nagu pamoja na kumpongeza Mkuu wa wilaya kwa jitihada zake za kulinda naa kuhifadhi mazingira,lakini aliweka bayana kuwa kama kuna jambo ambalo haliendi vizzuri katika wilaya hiyo ni suala la mazingira.
Diwani wa kata ya Hanang,mjini Peter Lori alionyesha kutoridhishwa na namna Halmashauri isivyoujali msitu wa hifadhi wa Mreru kwani kwa kipindi kirefu serikali imeitelekeza hifadhi hiyo.
Hata hivyo diwani huyo alifafanua pia kwamba inasemekana hifadhi hiyo ni mapito ya wanyama na kuhoji kwamba ni lini Mkuu wa wilaya hiyo atafikiria msitu wa hifadhi Mreru  utakuwa hifadhi ya Halmashauri ya wilaya hiyo.

HALMASHAURI HANANG YAKABIDHI HUNDI YA MIL.20 KWA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WALEMAVU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Fahamu Makundi Mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa - Sehemu ya Pili

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Habarini Wadau pokea codes kwaajili ya kuendeleza kutoa darasa la ufugaji bora wa Mbwa
Picha/Makala na Josephat Lukaza
Siku ya Leo tutaangalia Makundi mawili yaliyobaki katika makundi mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa, Siku zilizopita Katika makala ya Fahamu Makundi Mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa - Sehemu ya Kwanza tuliweza kuangalia Makundi mawili ambayo ni Viral Infections pamoja na Bacterial Infections. Leo tutaangalia makundi mengine mawili ya mwisho ambapo tutapata nafasi ya kuangalia ni magonjwa gani yapo katika Makundi hayo mawili yaliyosalia.
Yes Let's Back to Class kama wasemavyo Wazungu, Leo tutaangalia Makundi Mengine Mawili ambayo ni Kama Ifuatavyo
1: Fungal Infections
Fungal infections ni magonjwa ambayo  husababishwa na fangasi magonjwa haya yanaathiri binadamu pamoja na mbwa japokuwa Mbwa hushambuliwa mara kumi zaidi ya binadamu kwa magonjwa yasababishwyo na fangasi. Magonjwa yasababishwayo na fangasi kwa Mbwa yanaweza kuleta madhara katika Macho, Ubongo, ngozi nk. Katika Kundi hili la magonjwa yasababishwayo na fangasi Ni kama vile Blastomycosis, Histoplasmosis,

RC MNYETI AWASHUKIA MAHAKIMU MANYARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Wananchi wa Mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakitoa kero kwa Mkuu wa Mkoa huo Alexander Pastory Mnyeti. 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro. 
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amewataka mahakimu wa mkoa huo kutekeleza wajibu wao ipasavyo wakati wanaposikiliza kesi na kutoa hukumu kwa haki ili kuepuka malalamiko yanayotolewa na wananchi. 

Akizungumza kwenye ziara yake ya kwanza ya siku saba katika Wilaya ya Simanjiro, Mnyeti alisema kupitia nafasi yake ya Mwenyekiti wa kamati ya maadili, hatakubali kuona wananchi wanalalamikia kukosa haki. 

Mnyeti alisema baadhi ya mahakimu wanajigeuza kuwa miungu watu na kushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo hivyo kusababisha malalamiko kwa wananchi. "Hatuwezi kukubali kuona mambo kama hayo, yakifanyika kama kuna mtu anaona kuna mahakimu siyo waadilifu wanakula rushwa na kushindwa kutoa haki nijulisheni," alisema Mnyeti. 

Awali, mkazi wa mtaa wa Njiro, Theopista Paulo alisema amekuwa akinyanyasika wakati akidai haki yake. Theopista alisema mmoja kati ya mahakimu wa eneo hilo alikuwa anamwambia hata kama akimkataa na kesi yake kuhamishwa kwenye mahakama nyingine hawezi kushinda chochote. 

Hata hivyo, Mwanasheria wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo, Peter Mangala alisema mwananchi yeyote ana haki ya kumkataa hakimu endapo atakuwa na sababu za msingi. Mangala alisema endapo mwananchi akiwa na hoja za msingi anazozipinga anaweza kumkataa jaji au Hakimu atakapobaini kuwa hawezi kutendewa haki.
 

WANACHAMA 139 WA CHADEMA SIMANJIRO WAJIUNGA NA CCM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

WANACHAMA 139 wa Chadema wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wamejiunga na CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Manyara Mosses Komba. 

Akizungumza wakati wa kuwapokea na kuwakabidhi kadi za CCM wanachama hao wapya, Komba alisema wamefanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Komba alisema hawatajuta kujiunga na CCM kwani hivi sasa chama hicho kinachoongozwa na Mwenyekiti wake Rais John Magufuli kinawatumikia wananchi kwa kutatua kero na kuufanikisha maendeleo. 

Alisema wanakaribishwa CCM kwa moyo mmoja hivyo washirikiane na wanachama wengine ili kuhakikisha wanalirudisha jimbo hilo na kata sita zinazotawaliwa na Chadema. "Kati ya makosa tuliyofanya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ni kuachia jimbo la Simanjiro liende Chadema na kata za Mirerani, Naberera, Loiborsiret, Ruvu Remit, Loiborsoit na Endiamtu zichukuliwe na wapinzani," alisema Komba. 

Alisema ushabiki wa kufuata mkumbo ndiyo uliowagharimu wananchi wa wilaya hiyo na kata hizo, hadi kusababisha wakapatikana madiwani na mbunge wa kutoka upinzani badala ya CCM."Nakuagiza Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya ya Simanjiro, Thomas Mollel na wenyeviti UVCCM wa kata husika ambazo madiwani wao ni wapinzani, mkishindwa tena 2020 mjiuzulu," alisema Komba. 

Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya ya Simanjiro Thomas Mollel alisema kwa kushirikiana na vijana wenzake wa Simanjiro, watahakikisha wanatekeleza agizo hilo la kurejesha jimbo na kata sita zinazoshikiliwa na wapinzani. "Hata hivyo, wananchi wengi wa Simanjiro wana imani kubwa na Rais John Magufuli kupitia CCM mpya, tunatarajia uchaguzi ujao wa mwaka 2020 tutarudisha jimbo na kata hizo sita," alisema Mollel. 

Alisema vijana ndiyo nguzo kubwa ya ushindi kwenye chama hicho na wamepata mwamko wa kushiriki kuwajulisha wananchi kuwa CCM ndiyo chama cha kukimbilia. Mjumbe wa baraza la utekelezaji UVCCM mkoa wa Manyara, Elizah Ladis alisema tangu waanze ziara ya kutembelea wilaya za mkoa huo mwezi Desemba mwaka jana, hiyo ndiyo idadi kubwa ya wapinzani 139 kujiunga na CCM. 

"Simanjiro wametupokea kwa wapinzani 139 kujiunga na CCM wilaya za Hanang na Mbulu, wapo waliojiunga ila siyo wengi kama hawa, tunaelekea Kiteto na Babati sasa tunatarajia kupata wapinzani wengine," alisema Ladis.

SIMANJIRO YAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 25.3

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Leskar Sipitieck akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo baada ya kupitisha mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 25.3 kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 kushoto ni Makamu Mwenyekiti Albert Msole na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Zuwena Omary na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Yefred Myenzi. 
 
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 25.3 kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019. 

Akizungumza baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Jackson Sipitieck alisema vipaumbele vya bajeti hiyo ni elimu, afya, maji na viwanda. 

Sipitieck alisema suala la kupitishwa kwa bajeti ni jambo moja na utekelezaji ni jambo lingine, hivyo kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake ipasavyo wakiwemo madiwani na watumishi, ili kufanikisha hilo. Alisema kila mmoja kwa nafasi yake akisimama kwa nguvu zote, wilaya ya Simanjiro itapiga hatua kubwa ya maendeleo na wananchi wake watakuwa wanapata huduma zao za kijamii kwa ufanisi mkubwa zaidi. 

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi alisema bajeti hiyo ni kwa ajili ya matumizi mbalimbali, ikiwemo miradi ya maendeleo, ruzuku ya uendeshaji ofisi na mishahara. Myenzi alisema wilaya hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha wanaboresha vipaumbele vyao vya elimu, afya, maji na viwanda. Alisema mazao ya mifugo, ikiwemo maziwa, ngozi na nyama inapaswa kuboreshwa ili iwe chachu ya vichocheo vya uchumi. 

Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary aliwapongeza madiwani wa halmashauri hiyo kwa kupitisha mpango huo wa bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa manufaa ya wananchi. "Pamoja na hayo tunapaswa kuhakikisha tunatekeleza agizo la kila mkoa kuwa na viwanda 100 kwa sisi Simanjiro kuanzisha viwanda 15 ambayo vitasambazwa kwenye kata zetu na vijiji," alisema Omary. 

Hata hivyo, Diwani wa Kata ya Komolo, Michael Haiyo aliipongeza bajeti hiyo na kusisitiza ikamilishwe kwa vitendo. Haiyo alisema bajeti hiyo imegawanywa bila upendeleo kwani kata zote zimepatiwa miradi ila umuhimu wake utaoneka endapo itatekelezwa kwa vitendo. Diwani wa kata ya Naisinyai, Kilempu Ole Kinoka alisema bajeti hiyo inapaswa kujali suala zima la uboreshaji wa mifugo kwani asilimia kubwa ya wananchi wa eneo hilo ni wafugaji. 

"Sisi kwetu kahawa ya Simanjiro ni mifugo ambayo ni roho ya uchumi, hivyo tunapaswa kulizingatia hilo kwenye utekelezaji wa bajeti yetu," alisema Ole Kinoka.
 

KUELEKEA DESEMBA 9, 2017: SISI NI TANZANIA MPYA+

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
 
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa